PENZI LANGU 09



 PENZI LANGU 09

Suma aliamka asubuhi kama kawaida yake na kumuandalia Nadya supu kisha akaenda kumuamsha Nadya aliamka na kuoga maji kisha akatoka sebleni akiwa amepndeza mwenyewe akamuaga Suma kua anaondoka Suma akamuhulizia


"Nadya Kila siku huondoki bila kunywa chai na Leo nimekuandalia supu kwaajir ya pombe ulizokunywa Jana"




"Suma sijiskii kula Chochote badae bwana"


Nadya aliondoka zake na kumwachia Suma mwenye mawazo sana akachukua simu yake na kumkuta missed calls za Aisha akazifuta na kumpigia lafiki yake juma wakakutana hapo kwenye duka la vifaa vya magari na akamuhulizia


"vipi Ile hela ambayo nikikuelekeza umefanya kama nilivyokuambia?"


"yaani Suma mbona Bado kidogo tu kila kitu kinakua sawa"




basi Suma baada ya kumaliza kuzungumza na juma alitoka Hadi kwenye matengenezo na kumkuta Kila mtu Yuko bize na kusimamia matengenezo ya sehemu ya kuosha magari.




wote walismhukuru sana Suma Kwa moto aliokua nao wa kuwainua kutoka pale walipokua Suma akawambia kua wasijari Kwa Chochote kile.




Suma alirudi nyumbani mapema na kuandaa chakula vizuri na kukihifadhi kwenye hotpot kisha akwa anaangalia movie.




siku hiyo nadya alichelewa sana kurudi Suma alilala pale pale Hadi alishtuka baada ya kung'atwa na mbu na baada ya kumtazama saa ilikua saa7 usiku Bado Nadya hajarudi nyumbani ikabidi achukue simu kwaajir ya kutaka kumpigia simu iliita na kukatwa muda huo huo na baada ya muda mfupi Nadya aliingia ndani akiwa amelewa Tena kama siku iliyopita Hali ambayo ilikua inampa mashaka sana Suma.




aslimama na kwenda kumdaka maana akitaka kuanguka na kuumia vibaya kutokana na viatu virefu alivyokua amevaa.


sum aliumia sana kutokana na Ile Hali basi alimbeba na kumpeleka chumbani Tena na kumlaza kitandani huku alizungumza


"nadya hiki unachofanya unanifanya niogope sana na mbona umebadirka ghafla niambie kama numekisea nijirekebishe lakini sio kunitenga na kunifanyia haya yote mkewangu kumbuka mimi ni binadamu pia Nina moyo Nadya tafadhali"




nadya aliziba maskio yake na kugeuka upande wa pili kulala zake kitendo ambacho kilimuumiza zaidi sum basi hakua na namna akarudi sebleni pia akalala.




hiyo ilikua siku ya jumatatu na ikumbukwe kuwa tayari Nadya alishatumiwa ujumbe na mpenzi wake kua baada ya wiki moja anarudi hivyo hatujui huyo ni mpenzi wake au ndio kama alivyomwambia Suma kuwa alimsaliti.




upande wa Aisha hakua analala sababu ya mipango yake ya kuhusu kuripa kisasi na kilichokua kinamuwazisha ninani ayamuamini kufanya nae kazi maana limuamini sana mpenzi wake Suma lakini amehisi kua amemsaliti lakini hii siri ya Suma kumsaliti Aisha tunaijua Mimi na wewe ndugu msomaji ila Aisha na mama yake wote hawajui ispokua Aisha anahisi kutokana na vijitabia mbalimbali.




"kama Suma ameweza kunisaliti nani naweza kumuamin Kwa kufanya nae kazi ya kuripa kisasi,na pia najua kua nikazi ngumu haitahitaji vijana wavivu na najua pia itatumia pesa nyingi saña lakini sijali kuhusu Hilo nia na malengo yangu ni kuripa kisasi tu na lazima nifanye hivyo"




Aisha alichukua simu yake na kubofya sehemu kadhaa kisha akaweka simu sikioni kwake na simu iliita na kukata yenyewe na baada yakutama muda akatabasamu na kusema


"eeh kumbe ni usiku wa saa7 mmh aise lazima ndiomaana hajapokea itakua amelala"


Kisha nae akavuta shuka na kulala zake.




asubuhi mapema Aisha aliamka akavaa traki na vest yake na raba akatoka bila ya kumuaga mama yake Suma.


na upande wa Suma aliamka mapema kama kawaida yake kuandaa kifungua kinywa kwaajir ya nadya na aliamka na kuaga maji na kuondoka wakati huo Suma alikua bize na kazi zake nyingine na alivyorudi chumbani kwaajir ya kutaka kumuamsha Nadya hakumkuta na alipojaribu juangaza kote hakuona hata gari ya nadya alikua anajihuliza sana saña na ilizidi kumfanya ajionee sio wathamani Tena hivyo akajisemea


"najua Sasa nimechoka sana ndiomaana haya yite hutokea huyu sio Nadya ambae nimenzoea siku zote wanasema jiongeze kabla haujaongezwa hivyo hapa akili imo kichwani mwangu Sina muda wa kupoteza Tena.




alichukua simu yake na kubofya sehemu kadhaa ya keypad yake na kuweka sikioni kwake.




upande wa Aisha alikua kando ya barabara alikimbia na kufanya mazoezi ya viungo akiwa na hasira sana mara alipita kijana mmoja ambae nae pia alikua anafanya mazoezi akamwambia


"usitumie nguvu kufanya mazoezi maana utafanya mili wako uchoke kupitiliza"


"ahaa asatne sana kwa ushauri wako"




mara simu ya Aisha ikaita alifungua zipu ya traki yake na kutoa simu Kisha kupokea bila ya kutazama nani alikua anapiga ikasikika tu sauti


"mama shikamoo..!"


"marahaba Suma lakini Mimi sio mama yako"


"Aisha unathubutu vipi kuitikia Kwa kujiamini hivyo we mjinga sana Yani niambie mama yangu yupo wapi?"


"aah Sasa Suma Naina umeota mapembe enewei kama unahitaji mama yako basi moigie kwenye simu yake mjinga mmoja wewe"


Aisha alikata simu na kuiweka kwenye traki yake na kuendele na mazoezi yake na yule kaka akiendelea kumsemesha


"kwanini unafanya mazoezi Kwa hasira nahisi Kuna jambo unapanga kufanya kama sikosei"


"yeah nikweli lakini hayakuhusu"




yule kaka ilibidi awe kimya Kwa muda kisha kumuacha Aisha akiendelea kukimbia Kwa kwenda mbeke na kurudi nyuma lakini mara ghafla wakati anarudi nyuma kuna gari ilitokea nyuma yake na kumpush Aisha na kumfanya aanguke chini kwa kukosa pumzika kutokana na mazoezi ambayo alikua anayafanya yalikua yananguvu sana na yeye alikua anatumia nguvu na hasira pia.




na wakati like jambo limetokea yule kaka ambae alikua anamsemesha Aisha aliona na haraka akawahi kumbeba na kumwambia aliyemgongaa ampeleke hospital na hakua mwingine alikua ni Nadya kutokana na msongo wa mawazo kichwani kwake.




walifika hospital na baada ya kumfanyia vipimo akagundulika kuwa yupo salama ila alizima kwaajiri kukosa hewa mshtuko Yu lakini hakua ameumia,Nadya alifurahi sana maana hakuwahi kupata kesi ya kugonga hivyo alikua muoga sana.




baada ya kupata nafasi ya kumuona Aisha alimuomba msamaha na Aisha akamwambia Hana tatizo amemsamehe tayari kisha akaripia gharama za hospital na kuondoka zake.


Aisha alibaki na ye kijana Sasa wakati huo tayari walikua wanatoka hospital wakiwa wanatembea kawaida yule kijana akajitambulisha


"naitwa Samuel"


"naitwa Aisha ila kwanini ulinisaidia wakati nilikujibu vibaya kabla?"


"Aisha tunatakiwa kuwa na moyo wa ubinadamu sawa wewe ulinijibu vibya lakini Mimi sikutaka kukufanyia ukatili wa kutokusaidia sababu nisingepata faida yoyote kama ungekua umeumia alafu sijakusaidia,lakini nimekusaidia nimepata kufahamiana na wewe"


"ooh nikwi pia nisamehe kwa kukujibu vibaya"


"usijari kuhusu Hilo Aisha lakini nataka kukukaribisha nyumbani kwetu Kuna gym pia unaaeza.kuja kufanya mazoezi yote unayotaka wewe"


Aisha alitabsam na kumuhuliza


"serious unachosema?"


"ndio karibu sana najua pia itakua nafasi kubwa sana ya kufahamiana kwa ukubwa zaidi"


"Asante saña unaonekana mkarimu sana Samuel.."


Aisha alimtajia namba ya simu Kisha waachana kwenye njia panda na Kila mmoja kuelekea nyumbani kwao.




alidika nyumbani kwao majira ya saa6 mchana akamkuta mama yake na Suma amekua nawasiwasi alimsalimia na kutaka kuingia chumbani kwake mama Suma akamwambia


"kwanini unanikwepa Aisha?"


"mama kwanini nikukwepe mama?"


"Aisha umekua hivyo Kwa muda hata Mimi aliona ndiomaana nakuhuliza shida Nini?"


"hakuna shida yoyote mama ni mawazo yako tu hayo"


"Sawa unatoka wapi sasahivi na hunavaa hata nguo huko juu?"


"mama nimeanza kufanya mazoezi yangu Sasa na nitakua natoka Kila alfajiri ila bahati mbaya nikipata ajari kidogo ndiomaana nimechelewa Leo"


"ajari Gani Tena mwanangu ona Sasa jamanii"


"usijari mama ilikua ya gari lakini sijaumia ndiomaana nipo hapa"


"pole sana mwanangu nenda kaoge uje kula"


Aisha aliingia chumbani kwake akajimwagia maji na kujilaza kitandani kwake.


hatimae siku ya jumanne ilifuka usiku ndipo Aisha alimaka na kumwambia mama yake kua anaijiskia vizuri akachukua simu na kumpatia mama yake na kumwambia


"Suma alipiga akataka kuzungumza na wewe mpigie"


mama yake alichukua simu Aisha akawa Yuko bize kutengeneza maziwa ya unga kuweka maji ya moto kisha akachukua na mkate akaanza kula huku alijifanya yupo bize na tv.




mama yake na Suma akawa anongea na simu na mwanae


"mama uko sawa kweli?"


"Suma nipo Sawa na Aisha ananijari sana kwani shida Nini?"


"mama nataka kurudi nyumbani mimi maisha ya huku yamenishinda Sasa sitaki tena kuwa huku"


mama yake Baada ya kuskia hivyo mama yake akamuita Aisha Hadi Aisha alishtuka na kujikuta akimwaga maziwa yake na kumfata mama yake na kumuhuliza


"shida Nini mama?"


"Suma anataka kwenda kijijini"


Aisha alikata simu na kumwambia mama yake mama umeshaharibu najua Suma ameshakusikia tayari aaha"


Aisha alichukua simu na kuingia nayo chumbani,kitu ambacho kilimshangaza sanaa mama yake Suma akasogea sebleni na kumkuta maziwa yamemwagika akasafisha na kurudishwa kikombe kwenye vyombo vichafu.


upande wa Suma alianza kumtumia ujumbe Aisha kumuhuliza kuhusu alichokisema mama yake Aisha hakua amejibu meseji hata moja ya suma"


muda ulizidi kwenda Kwa kusubiri ujumbe kutoka Kwa Aisha na Huku akimsubiria pia Nadya.


siku hiyo alisota sana kusubiri vitu viwili Kwa wakati mmoja Hadi inafika asubuhi hakuna chochote alichokipata.


Suma siku hiyo akachukua karatasi na peni kisha akaandika walaka mzito sana na kisha akachukua nguo zote ambazo alikua amempatia Nadya na kuviweka kitandani kisha akatoka nnje na kufunga mlango na kuondoka zake hakuchukua kitu chochote zaidi ya kama vile alivyokua amekuja.




alifika dukani Kwa juma na kumwambia


"juma rafiki yangu pesa ambayo umekua ukiniwekea kwenye akaunti yangu inatosha sana kaunzia Sasa Kila pesa ambayo itakua unaipata hapa dukani ni yako na pia hili duka nilako na kule car wash utawachia rama na wenzie Mimi wacha nirudi nyumbani kwetu"


"Suma unamaana unarudi Kijijini?"


"ndio juma narudi kijijini kwetu"


"hapana usifanye hivyo Suma mbona tayari umeshaanza kutengeneza pesa nzuri tu jamanii?"


"usijari juma kwaheri kama Mungu akipenda tutaonana"


unadhani itakuaje usikose itaendelea....