PENZI LANGU 06


Hatimae wasafiri walifika salama jijini dar es salaam na Moja Kwa Moja gari ilielekea maeneo ya msasani ndiko ambapo kulikua na nyumba Yao ambayo watu wengine hawaifahamu.




yule dereva akamwambia




"dada Aisha nimekuleta hapa sababu ndio sehemu salama kwako hivyo utaishi hapa Huku tukiendelea kufanya kitu kizuri kwaajir Yako"




"aah sijaelewa unamaana Gani kusema hivyo kwani Kuna kitu gani nyuma ya hili ambacho sikijui?"




yule dereva aliona anaelekea kujaribu mipango hivyo akajikuta anampoteza Aisha Ili asishtuke akajifanya kumuhuliza




"KUMBE Bado unawasiwasi na kilichotokea?, usijari dada Aisha ni muda mrefu sasa umepita na usichokijua ni kwamba hao waliohusika tayari wameshatiwa kizuizini hawawezi kukufikia Tena"




"ooh Dan nenda tuachen tupumzike kwanza"




"Sawa dada Kila kitu kipo stoo ila ukihitaji chochote nipigie simu nitakuja"




"Sawa kwaheri"




Dan aliondoka na kuwaacha Aisha na mama yake Suma ,Aisha akamwambia mama mkwe wake




"mama hapa ndio nyumbani na tutaishi hapa"




"nyumba ni nzuri sana lakini ipo kimya sana"




"nikweli mama sababu hakukua na mtu yoyite ambae anaishi hapa tangu wazazi wangu wamefariki ilikua imefungwa tu na hatukua tunaishi hapa kabla,tulikua tunaishi kwenye nyumba nyingine huko masaki"




"ooh wazazi wako walikutengezea mazingira mazuri sana binti ila vijana wenye roho mbaya ya kwanini ndio iliyowafanya wateketeze familia Yako pole sana"




"Asante mama na sitaki kukumbuka kile ambacho kimetokea nataka kuanza upya na familia yangu mpya ambayo ni wewe na mpenzi wangu Suma sababu nawapenda sana"




"Aisha Wacha tu nikwambie kua na sisi tunashukuru sana Kwa ujio wako umetuvumbua mambo mengi sana pia hata akili zetu pia umezinyoosha kutokana kutotaka kutafuta amenedeleo kwenye maeneo mengi sababu ya uoga lakini Suma pia alikuaa muelewa kwako na akaamua kutuacha na kuja Huku bila ya uoga japokua ilimuwea vigumu sana kutuacha watu ambao anatupenda lakini hakua na jinsi"




"mama usijari kuhusu Hilo naamini kua Suma ridhiki yake kama iliandikwa atapata Kwa kuja mjini basi atapata mafanikio makubwa sana"




"nikweli mwanangu,ila tuachane na hayo ukweli nimechoka sana Nina uchovu mwingi sana nahitaji kupumzika"




Aisha alimpeleka chumbani na kumwambia




"utakua unalala Huku ndani siku zote na mimi nitakua nalala chumba cha pili kama ukiona huelewi utanishtua tu nitaamka hata atakaporudi Suma pia tutakua na furaha zaidi"




"Sawa mwanangu"




Aisha alitoka chumbani na kurudi seblen kisha akajilaza kwenye sofa Huku akikumbuka mambo mengi ambayo yametokea kipindi Cha nyuma Cha maisha yake.




alikua anawaza sana kuhusu kuripiza kisasi Kwa wale watu ambao wamemuulia wazazi wake lakini moyo wake ulijawa na wasiwasi sababu alikua anawaza kama ataianzisha vita upya atawapoteza Suma na mama yake hivyo ni jambo ambalo lilikua linamfikilisha sana.




""hahahaha Binti mrembo sana mashallah bwana Abdul na mkewake wamebahatika kupata Binti mrembo sana angalia macho yake kama mzungu pua yake mdomo wake angalia hata mwili wake pia,akiwa mkubwa atakua mtam sana huyu,hahahahahah""




ni sauti ambazo zilikua zinajirudia kwenye kichwa cha Aisha na Huku alijaribu kukumbuka sura za watu ambao wamewafanyia ukatili wazazi wake.




aliamka kutoka pale seblen akaingia bafuni akajimwagia maji kisha akajipumziaha kitandani kutokana na kuchoka Kwa safari iliyokua ndefu sana.




Kwa upande wa Suma pia alimaliza kazi zake mapema sana kisha akajilaza kwenye sofa mara akasikia mngurumo wa gari Suma alijifanya amelala fofoo,mara mlango wa nyuma pia ukafunguliwa na nadya akaingiapia nakufunga mlango kisha akasogea Hadi karibu na Suma kisha aka m'busu kwenye paji la uso na kuingia chumbani kwake akajimwagia maji na kutoka sebleni akiwa na kanga yake nyepesi kama kawaid yake akasogea karibu na alipoegesha Suma kichwa chake na kutoa mto ambao amelalia na kumuweka kwenye mapaja yake huku akichezea nywele zake.








"mpenzi jamanii kulala Gani huko jamanii nimerudi mkewako"








Suma alijifanya kujinyoosha na kutaka kuamka Nadya akamzuia na kumwamkia




"sitaki uamke kipenzi yaani natamani hata nisiwe naenda kazini tuwe tunakaa hivi Kila mara nataka kuimarisha upendo wangu kwako Kila siku"








"ooh Nadya unanipenda kiasi Gani?"




"yaani Suma sijawahi kumpenda mwanaime kama navyokupenda wewe sababu kwanza ni watofauti na wengine hauna tamaa mpole mkarimu kifupi unanivutia saña"








"ooh asante saña kipenzi changu,ila Leo nimeandaa chakula kizuri kwaajiri yako"








"baby lakini nimeshiba tayaro Leo ofsini kulikua na...."




"nadya tafadhali nataka ule japo kidogo tu mkewangu"








Nadya alivyoitwa make Tena alifurahi saña na kukubali kula chakula alichopika Suma.




walikua huku story za hapa na pale zikiendelea Suma nikama akitaka kuzungumza kitu lakini alipokumbuka kihusu maneno ambayo ameyazungumza Nadya kuwa yeye ni mwanaime wa tofauti Hana tamaa ikabidi ajitulize na kile alichotaka kumwambia abaki nacho moyoni mwake.








walkkula chakula Hadi wakashiba na kuzima taa kwaajiri ya kwenda kulala.




usiku huo ulikua wa mawazo saña Kwa Suma sababu alikua na mipango mingi saña kichwani kwake na ya kupata pesa hivyo akwa anatafuta njia ya kumueleza Nadya kihusu mpango wake.








Asubuhi mapema kama kawaida Suma aliamka na kuandaa Kila kitu na kumuamsha Nadya wake akajiandaa kisha akatoka sebleni kwaajiri ya kunywa chai.




wakati Nadya anakunywa chai muda huo Suma alikua anasafisha viatu vya Nadya na kuviweka mlangoni na kisha akamsogelea na kumwambia




"Nadya mkewangu Leo nataka kuwafanyia saplaiz marafiki zangu wakina juma sababu nimewamiss saña mana nilipotea machoni mwao tu ghafla na nataka nikwambie sehemu walipo Ili wasiwe na wasiwasi juu yangu"








"ooh Suma sitaki ukawambie sehemu ulipo kama unaenda tu kupiga nao story ni sawa ila sitaki uwambie ulipo Kwa Sasa"








"ooh kuhusu Hilo tu mkewangu ondoa shaka si unaniamini basi Wala hata usijali na sitachelewa kurudi,nitarudi mapema na kukuandalia chakula kama kawaida"








"sawa mpenzi wangu nakupenda saña Suma usiniache sawa mmewangu?"




"naanzaje kukuacha mwanamke mzuri kama wewe"




Suma akitaka kum'busu Nadya lakini ghafla simu yake ikaita hivyo hiko kitendo kikakatishwa na hiyo simu Kisha akapokea na baada ya muda mfupi alimuaga Suma Kwa haraka na kuondoka zake.




Suma alimshika kiuno chake na kusema




"chelewa Chewa utakuta mwana si wako Suma"




Suma aliingia chumbni na kuanza kupekua alifunga drop ya kitanda akakuta funguo nyingi akachukua zote na kuanza kufunguka kabati ambalo lilikua kubwa saña akafungua mlango wakwanza akakutana na nguo za kiume nyingi saña akafungua mlango wapi

li akakuta viatu vya Kila aina pia vya mwanaume na akaendelea kufunguka milango yote na mwisho kabisa akakutana na kisanduku akakifungua pia na alichokikuta kilimfanya astaajabu saña na kumfanya ashangae saña.








usikose itaendelea....