PENZI LANGU 04
Nadya Baada ya kufungua mlango akakutana na mzee akamsalimia na kumwambia
"mzee kigo umenishtua sana kwakweli kaka unavyojua naishi mwenyewe humu ndani alafu ulivyogonga huo mlango nimeogopa Sana"
"aah samahani mjukuu wangu lakini Kuna muda uliniambia nije ila sijakukuta nilikuja kukwambia kua tayari kazi ulinipa nimemaliza na hiyo hela nilikua nahitaji Kwa haraka sana"
"ooh Sawa babu ngoja nikupatie ,kweli ndio nimerudi muda mfupi tu Leo nilikua na kazi nyingi sana"
"napenda mabinti wanaojituma kama wewe lakini kwanini unaishi pekee kwenye hii nyumba"
"usijali babu hivi karibuni nitaanza kuishi na mtu usijali"
"anha nilijua hakuna kabisa nilitaka kuja kuhamia"
Nadya alicheka sana Huku akifunga mlango na kuanza kumuita Suma
"Suma..! Suma...!,uko wapi em njoo bwana"
Suma alitoka alipokua amejificha Nadya alicheka sana na kumwambia inamaana kama kingenitokea kitu kibaya wakati mwanaume upo ndani kweli Suma?"
"hapana madam boss unajua...."
"Suma ukitaka kunikwaza niite Tena hilo jina"
"Sawa samahani lakini nimeshazoea,ila tuachane na hayo lazima nijirinde sababu jinsi ulivyo alafu unasema nyumba yote hii uko peke Yako huwezi kuamini hivyo nikajua Moja Kwa Moja nimefumaniwa nikaamua kujificha kujiokoa"
"Suma Sina mume Wala mpenzi nimeamua kufokasi kwenye kazi kuliko mapenzi na Kila napojaribu naona mauzauza tu ndiomaana nikaamua kuwa hivi"
"Sawa bwana hongera"
"Asante kwahiyo utakula Tena au niondoe vyombo?"
"aah hapana nimeshahisi nimeshiba tayari"
"basi Sawa Kaa pale ungalie movie"
Suma alikaa kwenye sofa wakati huo Nadya anaondoa vyombo mezani kisha akaingia chumbani kwake akaoga maji na safari hii alivaa khanga nyepesi kabisa tofauti na mwanzo alioga na kuvaa tenge na tisheti lakini Baada ya kula alioga Tena na kuvaa khanga nyepesi na kutokea sebleni wakati huo Suma alioga na vuaa Tena nguo zake zilezile.
Nadya alivyotoka chumbani akaja kukaa kwenye sofa karibu na Suma,Suma alikua bize kuangalia movie hakumtazama kabisa Nadya na hakuweza kujua Nini amevaa alikua mshamba wa TV hakuwahi kuangalia tv Kwa uhuru tangu azaliwe.
nadya alivyoona Suma hamjali Yuko bize akamshika kifuani kwake na kumwambia
"Suma muda umeenda twende basi ukalale"
"aah hapana Wacha tu nitalala hapahapa usijali"
"Suma naogopa kulala pekeangu bwana"
Suma alivyoskia sauti ya madeko kutoka kwa Nadya ikabidi Sasa amtazame Nadya kwanini kazungumza hivyo.alivyotupa jicho akamuona Nadya mwili wake ,na hasa pale jinsi alivyokaa na kile kikanga kifupi hivyoasilimia ya mapaja yake yalikua nnje Suma akishindwa hata kupepesa macho Kwa kuyatamani maungo ya nadya na alipopandisha macho yake juu akakutana na chuchu zikiwa zimesimama ipasavyo Suma akajihusi msisimko wa ajabu sana na nadya alimgundua mapema sana Suma wa jinsia livyoonekana.
mara Ghafla kwenye ile movie ikasikika mripuko flani hivi ambao ulimfanya Nadya ajisogeze Kwa karibu zaidina Suma na kumkumbatia Kwa kungu Huku akiigiza kua anaogopa,Suma akishindwa kumtoa kwasababu tayari mambo yalishamuwea magumu kwake.
Nadya alijisogeza zaidi na kumkalia Suma mapajani kwake na kuchua rimoti na kuzima tv Kisha akaanza kumchezea vindevu ambavyo vilikua vimeota vibaya sababu ya kukosa pesa yaani Kuna ndevu za kimaskini na ndevu za kitajiri,afu Kuna ndevu za kukosa hela😁😁au basi...
Nadya alianza kucheza na ndevu za Suma mara aguse kifuani kwake Huku akicheza na mwili wake Suma wakati huo pia Suma hakua nyuma na yeye alikua anampapasa mgongoni kwake Hadi kwenye kiuno chake na kurudi juu mpaka pale walipoona tayari mambo Yako moto.
nashughuli ilianzia sebleni na kwenda kumalizika chumbani,hapo kila mmoja alikua hoi sana na haikuchukua mda mrefu Kila mmoja alipitia na usingizi.
upande wa kijijini pia mama yake na Suma alikua hazungumzi na Aisha kutokana nayale mambo ya kumwambia kuwa waende mjini lakini Kwa siku hiyo Aisha nae aliamua kuwa mbali kidogo na mama yake suma maana hakutaka kumkwaza Tena.
mama yake Suma akamuita
"Aisha kipenzi nisamehe sana kwa kile kilichotokea najua nawewe nimekufanya uwe mwenye mawazo lakini yote kutokana na uoga wangu,lakini Sasa nimefanya maamzi yangu mwanangu"
"mama usijali kuhusu hilo sijajiskia vibaya lakini sikua nataka kukukwaza ndiomaana nilianza kukaa mbali ,na Nina shauku ya kutaka kujua umeamua kipi?"
"Aisha mwanangu nimekubali kuungana nawewe kuelekea mjini"
Aisha alifurahi sana na kumkumbatia mama yake Suma Kwa furaha sana kisha akamwambia
"Asante sana mama kwa kunikubalia ombi langu na Nina furaha isiokifani natamani hata nikupe zawadi kwaajir tu ya kukubali ombi langu"
"usijali hata Binti yangu najua umepitia kipi na sikua nataka kufanya ukose furaha kwa kitu ambacho umekipanga pia najua ukiwa unafuraha wewe hata na mimi nakua na furaha hata mwanangu Suma pia atakua na furaha sababu mioyo yenu tayari ipo karibu na inafanya mawasiliano sana"
"kweli mama na natamani hata angelikua na simu nikamueleza hili lakini hapana ninataka kumfanyia saplaizi au unasemaje mama?"
"ndio ni vizuri sana natamani pia atafurahishwa na safari yetu"
"basi saa mama sasahivi ni usiku pumzika kesho tutapanga vizuri kuhusu safari yetu"
mama Suma akilala akiwa anatabasamu Baada ya kumuona Aisha anafuraha sana.
Asubuh mapema Suma aliamka na kujikuta amemkumbatia nadya Tena wakiwa uchi kabisa akataka kujitoa kwenye lile kumbato lakini Nadya hakutaka kumuacha Suma ndio alizidi kumkumbatia Kwa ukaribu zaidi kitu ambacho kiliamsha hisia za Suma upya na kujikuta wanapata Tena na cha asubuh kisha Nadya aliamka kwaajir ya kujianda kwenda kazini.
akiwa bafuni anaoga Suma alikua mwenye kujilaumu sana kwa kile kilichotokea na nadya Baada ya kutoka bafuni akamkuta Suma hayupo Sawa akamuhuliza
"mbona upo hivyo Suma unanini?"
"Nadya kwanini umenipitisha kwenye majaribu kwanini uliamua kufanya hivyo?"
Nadya alimsogelea Suma Kwa ukaribu na kumwambia
"ni kwasababu Moja tu Suma kwanza kabisa nilitamani kuwa na mpenzi Kwa muda mrefu lakini sikua nae sababu sikua na hisia na mwanaume yoyote lakini we nilipokuona Kwa mara ya kwanza tu moyo wangu ukaripukwa na upendo nikawa nashindwa jinsi ya kuanza lakini nashukuru mungu kwa kunipa ujasiri huu nilioupata kwaajir yako pia nimeinjoy sana na penzi lako maana sijawahi kuinjoy mapenzi tangu nianze kutajua ila wewe ndio fundi wangu"
"unaongea ujinga sana nadya Mimi Nina mpenzi wangu HUKO kijijini ananitegemea kwanini umefanya nimsaliti kwaajir yako?"
"ooh mpenzi kijijini? unajuaje kama yeye anaweza kujikontroo usijipe donda la roho Suma huwezi jua yeye huko kijijini anafanya mangapi changamka wewe au mie sio mtamu eeh?"
Suma alichukia sana na maneno ya nadya akasimama na kutoka zake nnje Nadya alitabasam na kumwambia
"I love you Suma na hapa ndio umeshafika huwezi kuniacha labda nitake mie"
Nadya alichukua handbag yake na kutoka chumbani na kumkuta Suma amekaa alisogea na kum'busu kisha akamwambia
"naondoka Suma mpenzi jla sitachelewa kurudi ukiwa na njaa stoo chakula kipo kwenye friji pia Kuna mahitaji pika ule usikae na njaa na sitaki utoke humu ndani"
Nadya aliondoka zake,Suma alibaki akiwa amekaa anawaza anawezaje kuishi hapo kuendelea kumsaliti mpenzi wake Aisha ambae anaempenda sana kuliko kitu Chochote.
ukweli ilimuwea vigumu saña Kwa upande wake na alikua na mawazo sana sana.ikanidi ajiinue na kwenda kuoga Ili kuufanya mwili uweze kufikilia jambo la kufanya tofaut na mawazo ambayo alikua nayo.
upande wa Huku kibaruani kwake matafiki zake walifika na Kila mmoja kumuhuliza mwenzake kuhusu Suma lakini kila mmoja alisema waliondoka kivyao wakiwa wanaendelea kubishana mara ilifika gari na akateremka mwanaume ambae ni yule jamaa ambae alimletea Suma kufanya kazi hapo akawahuliza
"nyie mwenzenu yupo wapi?"
"kaka sisi hatujui hata Yuko wapi lakini Jana tulimuacha hapa akisema kuwa anakusubiria wewe"
"ndio nilimwambia anisubiri lakini nikapitiwa sikuja kumchukua na hata nyumbani hakuja pia na Sasa basi kama amepotea au yukowapi atajua mwenyewe sihitaji kujua na nimekuja na nguo zake kifupi simtaki Tena nyumbani kwangu"
"lakini broo yule kama mdogo wako kwanini umchukulie hasira wakati ni mgeni huwezi jua amekumbana na Nini huko alipo"
juma alizungumza na wote wakatikisa kichwa kua wamekubariana na alichozungumza lakini jibu la yule jamaa nikuwa
"akija mwambieni kua simuhitaji kwangu hivyo myajua wenyewe jinsi ya kumsaidia"
Kisha karusha kifuko Cha nguo za Suma kisha akondoka zake na wakati ameondoka mara kuna gari ilifika pale na waliposogelea gari hiyo wakamkuta Nadya ambae ndo hupenda kumuita madam boss walimsalimia kisha akawahuliza
"nimeona yule jamaa binge hapa alikua anawafokea kwani ndio boss wenu?"
"hapana yule bwana ndio aliemleta Suma hapa na anasema siku ya tatu hajalala kwake na ukiondoa siku Moja ambayo alimkuta kala hapa hapa"
"MMH kwahiyo hata nyie hamjui Suma yupo wapi?"
"ndio madam boss tupo hapa tunajihuliza wapi alipo maana Jana tulimuacha hapa akimsubir yule jamaa lakini anasema alipitiwa na hakuja kumchukua haya nani mwenye makosa na ukizingatia Suma ni mgeni?"
"anhaa poleni sana washkaji zangu badae nitapita kwaajir ya kujua Nini kinaendelea kama amepatikana au lah"
"Sawa boss Asante Kwa kutuunga mkono"
Nadya alitoa pesa na kuwapa washkaji zake wakapate chai kisha akondoka zake bila ya kuwambia kua Suma yupo kwake...
usikose itaendelea...

0 Comments