PENZI LANGU 03
Usiku mzima Kwa upande wa Suma ulikua wa mateso kwasababu ya baridi kali sana na mbu walimshambulia sana Hadi inafika asubuhi.
Kwa upande wa yule jamaa ambae alimsaidia alipoamka asubuhi akawa anajiandaa kwaajir ya kuelekea kazini alivyotoka sebleni hakumuona Suma akamuhulizia mkewake
"inamaana yule dogo hajarudi Jana?"
"haha me nimesubiri sana arudi lakini sijamuona"
"mmh nawasiwasi sana kuhusu yeye na hij inawezekanaje?"
"hata me sielewi mumewangu"
"Sawa Wacha nijaribu kupitia pale nilipompeleka kwanza nitakupa taarifa"
basi waliagana na mkewake na kisha kuondoka zake.
alipofika kwenye eneo husika alimuona mtu kwa mbali akiwa amelala na ilikua muda ya sa12 asubuhi,alishuka kwenye gari na kumpiga hatua Hadi pale na kumuhuliza
"we Suma mbona umelala hapa shida Nini?"
"aah kaka za asubuhi?"
"nataka kujua mbona umelala hapa wakati nimekukaribisha kwangu au mkewangu amekuambia kitu Chochote kibayaa?"
"hapana kaka ila tu nilipotea na sikujua wapi Kwa kuingilia na pia Sina simu nikaamua nirudi kulala hapa maana hata wenzangu sikuwakuta"
"dah pole sana dogo vipi utafanya kazi au utaelekea kupumzika maana hapo ulipolala sidhani kama utakua Sawa kutwa ya Leo"
"usijali kaka Mimi nipo Sawa kabisa nitafanya kazi"
"poa basi jioni nitakupigia turudi nyumbani wote"
"asante kaka"
yule jamaa aliondoka na kumwacha Suma akiwa Bado kile kibaridi kinamtetemesha kidogo, alisogea kwenye benchi na kukata Huku akiwaza sana mbele yake itakuaje na tayari amewakumbuka sana mama yake na Aisha mpenzi wake.
mara juma na rama walifika na kumsalimia Suma aliitikia na kuwakaribisha na story iliwasigundue Chochote kuhusu yeye aliogopa kuchekwa,na hawakusubiria sana mara mwenzao mwingine alifika na kuendelea kupiga story.
upande wa kijijini kwao taarifa za vijana watatu kuchomwa moto ilifika kituo Cha polisi na Baada ya kuhoji chanzo Aisha yeye alikua msemaji hivyo akaona ni fursa ya kumuweka mbali mwenye Kiti hivyo alielezea Kila alichokiona Hadi sababu kuu ya kufanya hivyo na mwenye Kiti alifungwa Kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi maana hai vijana hawakupaswa kufa ila walipaswa kuolewa adhabu Ili wajifunze na kupewa nafasi ya pili lakini yeye hakutaka kuwaonya Wala kuwapa nafasi hivyo Kwa ushahidi tosha wa Aisha ulimfanya mwenye Kiti kuvuliwa cheo chake na kutumikia kifungo Kwa kosa la mauwaji.
mama yake Suma akamuhuliza
"Aisha mbona hukuwahi kuniambia kuhusu tatizo hilo huoni ni jambo kubwa na umenificha muda wote huo?"
"mama kumbuka haupo Sawa kiafya lakini pia najua kuwa ningekua nakuambia Kila kibaya nachopitia ningekua nakichosha Kwa mawazo mengi Huku uniwaze Suma Huku uniwaze mimi ukweli sikutaka uwe kwenye wakati mgumu mama"
"lakini Aisha...!!"
"mama usijali Mimi ni mtu mzima naweza kujimudu na isitoshe Kuna jambo nataka kukwambia nahisi utakubaliana na mimi"
"jambo Gani Tena mara hii tu tayari ushataka kunibadirishia mada?"
"hapana mama sio hivyo lakini nataka tu kukushirikisha,siwezi fanya maamzi bila kukuambia wewe"
"Sawa mwanangu niambie tu Wala hata usijali"
"mama nimeona kuwa Sasa ni muda sahihi wa Mimi kurudi mjini mama Tena sio mimi tu na wewe pia siwezi kukuacha hapa"
"unamaanisha nini,na unataka kwenda kufanya Nini wakati ulisema kuwa unawindwa?"
"nikweli mama lakini nimeongea na mwanasheria wa baba amenipa taarifa kuwa wote wakifanya kitendo cha kikatili Kwa wazazi wangu pia walifanya kwenye familia nyingine pia hivyo walishashtukiwa na Sasa wapo kwenye mikono ya sheria"
"Mimi naogopa sana kwenda huko mjini Aisha bora niishi hapa Kwa amani kama ilivyokua unasemaga mwanzo mwenyewe"
"nikweli mama na ninajua fika kuwa adui huwa wengi sana lakini sioni sababu Tena ya kujificha sababu Sasa hivi Nina nguvu kutokana na Nina family ambayo inanipenda sana"
"hapana Aisha siwezi kwenda naogopa kufa kabla ya kuona mjukuu wangu na nyie mkiwa kwenye sura mpya ya ndoa"
Aisha aliendelea kumbembeleza mama yake Suma Ili waende mjini lakini Bado mama yake na Suma hakua mlahisi kihivyo hivyo ikabidi amuache afikilie na akiwa tayari atamwambia lakini Aisha tayari akili yake ilishakumbuka mjini na kutamani kuyaona makaburi ya wazazi wake.
upande wa mjini siku nzima walifanya kazi kama kawaida Yao lakini Suma hakua vizuri Kuna hali flani ambayo alikua anajihisi Kwa muda lakini inakuja na kupotea kitu ambacho juma kilimfanya amuhulize
"vipi mzee wa bongo movie uko Sawa kweli?"
"hii juma inamaana ushampa jina mwenzio?"
"rama we huoni kama Suma ni muongo sana?"
"aah we juma ukianza kubishana humalizi ngoja tu niendelee na kazi yangu"
rama aliwaacha kisha juma akamuhuliza Tena juma na safari hii hakua ameleta Tena utani
"Suma Naina kama haupo Sawa Leo unatatizo Gani?"
"aah juma siko Sawa kabisa Yani ila naamini kua nitakua Sawa"
"pole sana kijana utakua Sawa"
basi walisaidiana kufanya kazi zao maana siku hiyo ilikua ya neema sana kwa upande wao maana magari yalikua yanasubiria foreni ya kuoshwa hivyo wote walifanya kazi kwa kujituma na bidii ya Hali ya juu sana.
mpaka inatimu jioni wote walikua wamechoka sana na kabla hawajao pumzika vizuri ilikua jgari nyingine kwaajir ya kutaka kuoshwa pia Suma akawambia
"kama mmechoka Wacha Mimi nioshe kisha tuondoka au mnaonaje?"
"Suma bwana Wacha iende tu hiyo gari maana kama unataka kuiosha Sawa ila sisi tunaondoka"
wale watatu wakaondoka na kumwacha Suma pekee Suma alianza kuliosha like gari Huku akisubiri kuja kufatwa na kaka yake hadi anamalizia kusafisha gari Bado kaka yake alikua hajafika
Suma alikua anatamani sana kwenda kupiga simu kinadhani ila alihisi akitoka tu pale ataibiwa hivyo alikua mtulivu sana paleoale Hadi inafika sambili usiku Bado huyo kaka yake hajafika.
ukweli ilikua inamuumiza sana kuzidi kuwaza kwanza mitaa haijui na simu Hana alikua na subra palepale.
mara Ghafla ilipita gari Kwa Kasi lakini Ghafla ilirudi na kupiga honi Suma aligeuka na kuhisi kua huenda ni kaka yake hivyo alisogea haraka eneo liliposimama gari lakini alipofika akamuona mwanamke akamsalimia vizuri yule mwanamke akashuka kwenye gari na kumuhulza
"nafikiri kama sijakosea wewe ni suma?"
"aah ndio ni Mimi umejuaje gari yangu?"
yule mwanamke alitoa miwani na kumwambia
"nilikuja Jana ukanioshea gari yangu"
"ooh madam boss..!!,sikuweza kutambua kama ni wewe kutokana na gari hii sio Ile ambayo umekuja nayo Jana"
"ndio lakini Mimi naitwa Nadya sio madam boss sababu hilo jina Hawa vijana ndio hupenda kuniita ila sio jina langu"
"anhaa sawa pia ni vizuri sababu kwanza linakupendeza sana"
"anhaa Asante pia lakini mbona uko mwenyewe wenzako wameenda wapi?"
"wao wameondoka lakini Mimi...."
"Suma haupo na sehemu ya kuishi sindio?"
Suma kama vile alipatwa na kigugumizi flani
"aah mi,ni ...aah"
"Suma usijali sawa ingia kwenye gari twende"
Suma aliangaza Huku na huko kisha akapanda kwenye gari ya nadya kisha Nadya aliwasha mziki na kuondoka maeneo yale Hadi nyumbani kwake.
Baada ya kufika nyumbani kwa Nadya Suma hakuacha kushangazwa na uzuri wa nyumba ambayo anaishi nadya na magari yalivyojipanga kwenye parking utafikilia kua ni ya watu au wafanyakazi wa kampuni husika,Suma akishindwa kuvumilia akamuhuliza
"inamaana Kila kitu unamiliki wewe madam boss?"
Nadya alimgeukia Suma na kumshika mabegani na kumwambia
"naitwa Nadya sitaki hilo jina,hata twende ndani"
Suma ilimbidi afunge Domo lake Huku aliendelea kushangazwa na uzuri wa bustani na mazingira ya Ile nyumba.
upande wa yule jamaa alirudi nyumbani kwake na kusahau kabisa kua aliagana na Suma kuwa ataenda kumfata.
alifika alioga maji Akala chakula na kuingiza kulala mkewake akamuhuliza
"mumewangu Leo ni siku ya pili shemeji Suma hajarudi lakini kwanini?"
"aah nimeshachoka Mimi pesa anapata anashindwa kujiongeza kuchukua boda boda hadi hapa nimechoka kumfikia bwana yule hanihusu Kwa Chochote kama anashindwa kujiongeza basi bwana Leo ndio mwisho wangu na kama hatirudi Tena itabidi tu nguo zake zichomwe moto kabisa"
"mumewangu sio vizuri lakini"
"ndio hivyo mwanaume gani unakaa nyua nyumba kama mifuko ya suruali achana nae na ulale sitaki kelele mimi hapa"
basi yule mwanamke aliamua kutulia na kuheuka upande wa pili na kulala.
humu Kwa Suma mambo ni moto maana nadaya aliandaa chakula kizuri Kwa haraka na kumkaribsha Suma mezani ,japikua alikua na kauoga flani lakini Nadya akamwambia
"kuwa huru humu ndani Niko mwenyewe tu usiwe na wasiwasi"
Suma japokua alitolewa wasiwasi lakini hakuweza kumuamin Nadya bado alijisemea mwenyewe kua wasiwasi ndio akili.
wakati wanaendelea kula chakula mara mlango uligongwa Kwa nguvu sana nadya aliaotwa na wasiwasi sana sababu tangu aanze kuishi hapo hakuwahi kugongewa mlango usiku Tena kwanguvu hivyo na hali ya wasiwasi wa nadya ilimshtua Hadi Suma pia ikabidi pia aache kula na kujificha jikoni,Nadya alipiga hatua Hadi mlangoni na kugusa kitasa Cha mlango Kwa kusita sana na kufungua mlango ....
usikose itaeendelea.....

0 Comments