PENZI LANGU 01


ANZA ...Mkoani tabora walionekana watu wawili ambapo Kwa kuwatazama tu ni kama vile walikua wapenzi ambao wamuda mrefu sana wakati huo mwanamke alikua ameshika kimfuko kidogo huku mwanaume akiwa ameshika mkono wake wakiwa wanatembea Hadi walipofika kwenye kituo cha treni mwanamke akazungumza


"Suma naomba sana usinisahau sababu nakupenda sana na nakutegemea wewe Suma kumbuka wewe na mama Yako ndo familia yangu kwasasa na kumbuka wapi umenitoa Suma nakupenda sana"


"Aisha usijali nakuahidi kua kidogo chochote nitakachokipata nitawatumia sababu sitaki mpate shida we na mama yangu kumbuka kua naenda mjini ni vile nahitaji kubadirisha maisha yetu sababu sitaki tubaki kuwa wakulima wadogo naenda kutafuta Ili tuweze kuwa wakubwa zaidi na wenye kutumia pembejeo za kisasa mpenzi"


"nakuamini sana na kama alivyokupa baraka mama Yako na mimi pia nakupa baraka zangu"


Aisha alikua anahuzuni sana kuagana na mpenzi wake ambae alikua anaempenda sana na kumheshimu Kwa kiasi kikubwa.


haukupita muda mrefu mara treni ambayo alitakiwa apande illifika na Suma alipanda kwenye treni akakaa kwenye siti huku akimpungia mkono mpenzi wake Aisha.


na watu wengine walipanda pia Kisha treni ikaanza safari yake kuelekea dar es salaam.


Aisha alirudi nyumbani kwao na kumkuta mama yake na Suma akiwa amekaa kinyonge Aisha akamsogelea mama yake Suma na kumwambia


"mama usijisikie vibaya naamini kua anatupenda sana hawezi kutuacha wenyewe hata kidogo naomba tuweke Imani kwenye hilo sababu tukiwa na mawazo mabaya itamuwea vigumu hata Kwa upande wake"


"nakuelewa sana Aisha usijali Mimi nipo sawa kabisa na nitafurahia sana endapo nitamuona kijana wangu Suma amerudi salama na kuja kufunga ndoa na wewe mwanangu mpole mwenye heshima"


"Asante mama ila wacha niandae chakula alafu niende shambani nikamalizie kupalilia shamba"


basi Aisha alifanya hivyo na kisha akondoka kuelekea shambani na kumuacha mama Suma nyumbani sababu alikua mgonjwa wa miguu hivyo alikua anapata shida sana kwenye kutembea.


wakati Aisha anaelekea shambani mara Ghafla akakutana na mwanaume mmoja ambae alionekana kua na maongezi na yeye Aisha alipomkaribia tu kabla ya huyo kijana kuzungumza akamwambia


"Joel naomba tafadhali niache nipite sitaki usumbufu wa aina yoyote maana ukiendelea kunifata fata nitakuja kufanya kitu kibaya sana"


"hahaha Aisha unaonekana kuwa na msimamo sana lakini safari hii nimekuja mwenyewe ila siku ambayo nitakuja tena nitakuja na wenzangu najua kihelehele chako kitakuisha"


"huwezi kunitisha Kwa Chochote kile na ukijifanya mjuaji na mimi nitakukomesha"


Aisha alimsukuma Joel na kuondoka zake,Joel alimshangaa sana kujihuliza

"huyu mwanamke anajiamini Nini na mbona mpenzi wake ambae alikua anamtetea ameshaondoka kwanini Bado anajiamini kiasi hiki,lakini pia yupo tofaut na wasichana wa hapa kijijini labda ndio maana anajiamini sana maana wasichana wa hapa ukimuonesha hata elfu Moja tayari washakubali unaipata show Yako Moja kisha unatulia ila huyu Sasa ni mgumu sana ila nitamkomesha siishii hapa"


Joel aliondoka zake.


muda ulizid kwenda hatimae jioni iliwadia Aisha alitoka shambani akiwa na mizigo yake na Moja Kwa Moja Hadi Kwa mwenye kiti akamsalimia na kumwambia


"samahani mwenye kiti ninashida nataka nikuambie"


mwenye kiti nayeye alikua anamtamani sana Aisha Kwa muda mrefu sana lakini Aisha alikua na msimamo sana hapo kijijini sababu alikua anampenda sana na kumuheshimu Suma kutokana na jinsi alivyompat na kumsadiia,hivyo mwenye kiti Kabla Aisha hajasema shida yake akamwambia


"Aisha kwanza vipi kuhusu nilichokuambia sababu mpenzi wako ameshondoka tayari"


"mwenye kiti sikuja hapa kwaajiri ya kujadiri hayo mambo nataka unisaidie Kuna vijana wananisumbua na wamepanga kunifanyia kitendo kibaya muda wowote ambao nitakua peke yangu nikienda shambani au kisimani pia"


"ooh jamani usijari kuhusu Hilo Aisha mpenzi nitashughulikia Wala usiwe na wasiwasi"


Aisha alisimama na kuondoka zake huku akimuacha mwenye kiti amejawa na tamaa za kimwili na yeye,Aisha alipoondoka mwenye kiti akasema

"yani huyu mtoto Kila nikikutana nae lazima tu niwe na mshawasha hivi ananini lakini ,ila mh mtoto mashallah anavutia Kila idara kwanza mweupe ana shape nzuri yaani daha natamani Ile siku ningemuokoa Mimi lakini ningewezaje sasa wakati nguvu ya kumtoa nilikua Sina,ila ananichanganya sana huyu binti lazima nimpate"


Aisha alirudi nyumbani kwao na kumkuta mama yake mkwe anapika Aisha akamuhuliza


"mama kwanini unapika SI nitapika Mimi jamani?"


"Aisha unafanya kazi nyingi Hadi nakuonea huruma ona sasahiv ulivyokonda wakati haukua hivi,Aisha kumbuka kua wewe hukutakiwa kuishi Maisha ya shida ila sema ndio hivyo hatuna uwezo"


"mama Mimi najiona heli ya umaskini wenye furaha kuliko utajiri wenye unaishi Kwa wasiwasi na tangu nifike hapa kwako nimekua na amani sana na furaha hivyo usijari mama"


"kweli unafuraha ukiwa kwenye Maisha haya?"

"zaidi ya sana mama na Wala usiwe na wasiwasi kuhusu Mimi"


basi Aisha alisogea kibandani na kuendelea na mapishi ambayo akiyaanza mama yake na Suma.


upande wa kwenye treni Suma alikua anawaza tu endapo atafika huko mjini ataishi wapi sababu Hana ndugu Wala jamaa hio kitu ilikua inamuwazisha sana akilini mwake.


baada ya siku tatu walifika jijini dar walishuka kituoni na Kila mmoja kuingilia sehemu anayoijua yeye.


upande wa Suma alikua hajui mitaa Wala hakua anajua wapi anaelekea alichojua yeye amefika dar basi Kambi yake itakua popote ambapo ataona patamfaa.


alitembea sana siku hivyo Hadi inafika majira ya jioni,akiwa zake maeneo ya kwenye soko la tandale mara ilikuja gari ambayo ilikua imepata hitilafu kidogo na dereva alishuka kwenye gari mara Moja na kutaka kutazama shida Nini akawa haelewi Nini afanye mara akageuka geuka na kumuonua Suma akiwa amekaa kinyonge akamuita


"oya we kijana njoo mara Moja"

Suma alisimama haraka na kusogea pale Kisha akaambiwa

"em niangalizie hapa mana sielewi hata"

kwakua Suma alishajifunza funza kijijini kwao jinsi ya kutengeneza magari pikipiki na baiskeri hivyo haikumuwea vigumu kugundua tatizo la kwenye hiyo gari,akatengeneza fasta na kumwambia


"jaribu kuwasha gari"


mwenye gari alifanya hivyo na mara hii gari ikawaka safi kabisa Suma hakutaka kuwa na pupa alifunga pale palipofunguliwa Kisha akasogea pembeni na yule jamaa alikua anaongea na simu na baada ya kumaliza akamuita Tena Suma alisogea na Kisha akamwambia

"shika hii pesa itakusaidia pia Asante Kwa kunitengenezea gari yangu"


"kaka Asante pia ila Mimi sitaki pesa nataka unisaidie kazi na sehemu ya kulala "


"ooh kumbe hauna makazi?"

"ndio kaka mi ni mgeni hapa ndio nimefika Leo tu kutoka tabora"


"ohk panda kwenye gari tuondoke"

Suma alikimbilia mfuko wake na Kisha kurudi Kisha akapanda kwenye gari na kuondoka na huyo jamaa.


gari iliendeshwa Hadi kwenye maeneo ya kinondoni Kisha gari ikapaki kwenye nyumba moja hivi Kisha akamwambia

"hapa ndo napoishi karibu ndani"

"Asante saña kaka"

waliingia ndani na Kisha wakapata chakula pamoja Kisha akamuonesha sehemu ya kuongea Kisha akampa shuka akalala seblen na yeye akaingia chumbani kwake.


Suma alimshukuru sana na kusema

"Asante mama Kwa Dua zako Mungu amejibu maombi yenu Kwa siku ya kwanza napata msamalia mwema wa kunisaidia wengi naskia wanapata shida sana kuhusu sehemu za kulala ila Mimi Leo nalala ndani Asante saña Mungu wangu"


Suma alilala pale seblen Hadi asubuhi mapema,aliamka na kuanza kupanga vitu vizuri mara ghafla mlango wa chumba ukafunguliwa na akatoka yule jamaa na mke wake akimuweka vizuri tai na kumchana nywele Kisha akazungumza

"dogo huyu ni mkewangu Jana sikukutambulisha sababu alikua amelala hivyo huyu mkewangu na pia mama watoto huyu ni yule kijana ambae nilikuambia hivyo atakaa hapa huku nikimfanyia mchakato wa kazi na sehemu ya kuishi"


"Sawa mmewangu,karibu sana shemeji"

"Asante saña"

basi walitoka nnje na kumwambia

"dogo sikia Wacha Mimi niende kqzini afu Kuna sehemu pale nitakuangalizia Kisha kesho utaanza kazi au hata Leo nitamtma mtu akufate"

"Sawa kaka hakuna shida"

yule jamaa aliondoka na kumwacha Suma na mkewake.


upande wa kijijini sasa Aisha aliamka kama kawaida yake na kuelekea shambani lakini akiwa njiani simu iliita na kuanza kuzungumza na hakua miwngine alikua Suma alifurahi sana kumskia na baada ya kumuhulizia mama yake akamwambia kua yupo shamba na muda ambao atarudi atamwambia Ili ampigie ukweli siku hiyo ilikua ya furaha saña Kwa Aisha na aliwahi kufika mapema sana shambani na kuanza kulima lakini ghafla walitokea vijana watatu na kumbeba Aisha mpaka mafichoni kwaajir ya kutaka kum'baka wakati wawili wanafanya doria kwaajir ya watu ambao watakaokua wanapita hapo mara ghafla.....


usikose itaeendelea....